Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo
imesema kifo cha shabiki huyo kimeacha pengo kubwa kwa nafasi yake
ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa pamoja na kuwa balozi mzuri
kama mwananchama wa timu hiyo.
Enzi za uhai wake Ally Yanga atakumbukwa
kutokana na mbwembwe zake alizokuwa akizionesha za kujipaka masizi ya
mkaa usoni pindi klabu ya Yanga ikiwa uwanjani.
Hata hivyo chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika.
Uongozi wa BONGO BASS unatoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na Klabu ya Yanga kwa pigo walilopata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni