Nikki amefunguka na kusema kwamba Mfalme huyo wa Salasala alibebwa na watu kwenye muziki na ndiyo waliomtupa na sehemu ambayo imemfanya ashindwe kuamka sababu inayomfanya hata kufikia kumtaja kwenye mahojiano mara kwa mara ili azidi kusikika.
"Zizi ameshushwa na
waliompandisha bila yeye kutarajia hilo. Ametupwa halafu ameenda
kuporomokea sehemu ambayo hata hajui atanyanyukaje, halafu ana watu wake
anahitaji kuwasema ila anaona Nikki mwanangu nikiongea nitammudu fresh,
kwanini awe muoga mbona mimi nawaambiaga,” Nikki alifunguka.
Aidha Nikki amejibu kauli ya Zillah
kumuita 'Wack' na kusema kuwa haelewi ni sababu gani zimemfanya msanii
huyo kutumia kauli hiyo huku akihoji labda kama anaishi maisha ya
kuigiza kama msanii huyo ingekuwa sawa..
'Ukiniita mimi 'wack' kwa
maana ipi, labda sijui kuandika, au 'wack' kama yeye hajui
anachokifanya? anaishi maisha ya kuigiza, kujifanya wewe unaisha maisha
ya Ulaya wakati upo Salasala unadanganya watu kuna all stars
zimeninginizwa kwenye nyaya za umeme whichi is not true. Ana stress zake
kaenda kwenye ufalme ambao sio wake sasa karudi huku ambako pengine
alitakiwa awepo amekuta wafalme ni wengine na sio yeye tena,” Nikki aliongeza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni