Z Anto anasema kuwa yeye ni kama baadhi ya wasanii ambao wamekuwa na maneno mengi kuliko utekelezaji ndiyo maana amekuwa akizidi kufanikiwa katika mambo yake licha ya kuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu.
Z Anto anakiri kuwa sasa anataka kurudi rasmi kwenye muziki ila hafanyi muziki ili kuendesha maisha yake bali anataka kufanya muziki kama njia ya kupanua biashara zake na kusema mpaka sasa kazi yake mpya imeshakamilika hivyo muda wowote anaichia.
"Mara nyingi wasanii huwa
wanakuwa na maneno mengi pasipo vitendo lakini kama tungekuwa karibu na
mazingira yangu ya biashara ningekwambia angalia aina ya biashara ambayo
naifanya labda ungepata jibu nafanya biashara ya aina gani lakini mimi
ni mmiliki wa fremu za biashara zisizopungua sabini na kitu hivi, lakini
pamoja na hivyo nina biashara zingine kama za magari, hata uongozi
wangu mpya ambao mimi nimeutengeneza utakuwa unadili na biashara kama
hizo na kubwa kuliko hizo tena lengo letu si kuingia kwenye sanaa
kutegemea show na dili za sanaa kama zilivyo hapana tunataka kuingia
kwenye sanaa tufanye kama wasanii wa nje wanavyofanya," alisema Z Anto
Z Anto aliendelea kusisitiza kuwa muziki ambao anataka kufanya sasa ni kama mtaji na kufungua njia za biashara zake zingine zaidi lakini si kufanya muziki kwa ajili ya kutegemea show tu peke yake, yaani anataka kutumia muziki kufungua milango mingine ya biashara.
"Wasanii wenzetu wa mbele
wanakuwa na kampuni sijui za maji, na vitu vingine wakati wakiendelea na
sanaa yao kwa hiyo hata mimi nataka kuingia kwenye biashara nyingi
tofauti tofauti kwa hiyo sanaa ni kama mtaji kwangu lakini tofauti na
hapo na biashara zingine za magari pia nina biashara zingine za
kifamilia nilikuwa nasimamia ndiyo zilikuwa zikinifanya kuwa busy kwa
muda mrefu kwa hiyo maisha yanakwenda kwa namna hiyo" alisema Z Anto
Mbali na hilo Z Anto anasema maandalizi ya kazi yake mpya yamekalimika kwa asilimia 98 kwani tayari ameshaunda menejimenti, ameshakamilisha video ipo tayari na kusema kila kitu kipo sawa kilichobaki ni kusema tu siku ya kazi hiyo ambayo inatakiwa kutoka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni