Baraka
The Prince amedai kuwa yeye hawezi kugombana na Alikiba na wala
hategemei kuja kumkosea kwa kuwa ni moja kati ya watu ambao wanampenda
sana yeye pamoja na sanaa yake.
"Unajua ukidili wa watu wa
Instgram wanaumiza sana kichwa kwa sababu mimi nipo kwenye label moja na
Alikiba, hivyo Alikiba ni brother wangu na naishi naye kama kaka yangu
kabisa, pia ni miongoni mwa watu ambao wananipenda sana, hivyo sitegemi
kuja kumkosea au hata kugombana naye sitegemi kitu kama hicho, sema watu
walianza kuongea hivyo baada ya kuona siongozinaye kama ilivyokuwa
kipindi cha nyuma, watu wamezoea kuniona kila anapokwenda Alikiba niko
naye kwa hiyo kuna sehemu zingine mimi sipo sababu sina sababu ya
kuwepo, Alikiba amekuwa ni mtu ambaye hapa nchini hakai sana kwa kipindi
hichi ndiyo maana wanakuwa hawaoni tupo pamoja" alisema Baraka The Prince
Mbali na hilo Baraka The Prince amesema
kuwa mkali huyo wa Aje hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya kuachia kazi
yake mpya baada ya Aje kusumbua zaidi ya mwaka mzima.
Alikiba na Baraka The Prince licha ya
kuwa chini la label moja ya RockStar4000 wasanii hao pia waliachia kazi
ya pamoja ambayo inafahamika kama 'Nisamehe'
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni