Nikki
amefunguka hayo ikiwa ni siku chache tangu kupata nafasi ya kuhudhuria
uwasilishwaji wa ripoti za mchanga wa dhahabu (Makanikia) Ikulu, na
kusema kwamba uwizi wa rasilimali haujaanza kufanyika leo hivyo ni vyema
Serikali ikaachia sehemu nyeti kama madini wakapatiwa watanzania.
"Ripoti zote zimeshaonesha
ni kwa jinsi gani tumeibiwa vya kutosha, hapa ningeishauri kwamba
makampuni yote yanayosimamiwa na wageni kutoka nje yataifishwe na wazawa
wakabidhile kuyaendeleza. Wawekezaji wanakwepa kodi kwa kusaidiwa na
viongozi pamoja na wanasiasa wanaowapunguizia hizi kodi hivyo kwa namna
moja au nyingine huu ni uwizi" - alisema Nikki
Nikki amezidi kwenda mbali kwa kutoa mifano kama "Kwa
mfano sehemu kama Bulyanhulu kulikuwa na wachimbaji wadogo wadogo laki
tatu amekuja muwekezaji mmoja wale wote wameondolewa walioajiriwa
hawafiki hata elfu kumi hivyo ajira zaidi ya laki mbili imepotezwa, hii
siyo tena uzalishaji wa ajira bali upokaji. sasa hivi Arusha hakuna
tena kina Papa King wapya kwa sababu ya wawekezaji walioingia migodini- Nikki aliongeza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni