Ditto
amefunguka hayo baada kuona watu wengi wameupokea vizuri wimbo huo na
kuchezwa sehemu mbalimbali huku wasanii wanaochipukia kuonekana na
wapotayari kufanya 'cover' kwa lengo la kuzidi kufikisha ujumbe mbali
zaidi.
“Watu wengi wanatamani
kufanya cover ya huu wimbo mimi naruhusu kiroho safi tu ila sasa wabongo
wasifanye kwa kuwauzia watu unajua mtu anapofanya 'cover' kwanza
kaonyesha kuikubali kazi hiyo…lakini sasa inapotokea mtu anataka kuuza
hapo ndipo anaharibu kazi…akifanya cover mimi namtazama kama msanii
mwenye kipaji cha ziada”. Alisema Ditto
Kwa upande mwingine Ditto amewashukuru
wananchi kwa kumpokea vizuri baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kabla
ya kuja na ngoma yake ya 'Moyo sukuma damu'.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni