Hutufanikiwa sababu ya chuki na wivu - Mesen

Msanii wa muziki wa bongo fleva na mtayarishaji wa muziki, Mesen Selekta amefunguka na kusema Watanzania wengi tunashindwa kufanikiwa katika maisha kutokana na wivu na chuki binafsi za watu.




Mesen Selekta amesema kuwa maendeleo yetu yanakuwa madogo kutokana na roho zetu mbaya, ubinafsi na chuki zisizo na msingi zilizopo ndani yetu. Mtayarishaji huyo amesema hayo baada ya mtayarishaji mwenzake wa muziki kusema kuwa Mesen Selekta anapoteza ladha ya muziki wa singeli.

"Sisi Watanzania maendeleo yetu yapo chini mno yaani ni madogo kwa sababu watu wengi tuna wivu na chuki ndani yetu, hata siku moja haijawahi kutokea producer yoyote kunifuata kuniuliza hata kunipigia simu au hata tukionana kuniambia au kuniuliza hivi Mesen Selekta singeli unatengenezaje. Mimi nilikuwa nasikia muziki wa singeli mtaani nikaamua kuchukua na kuufanya mpaka hapa ulipofika, lakini hao hao wanaongea walikuwa hawaupendi muziki wa singeli lakini saizi wakiusikia club wanacheza, tuache unafiki, tuache chuki, tuache wivu kinachotakiwa muziki wetu tuufikishe mbali" alisema Mesen Selekta


Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Social