Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza
toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao
walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.
Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha
Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume
wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.
“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako
wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara
watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana
nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen”
Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.
Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.
“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy.
Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la
kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Home »
» Mke wa Roma Mkatoliki atoa la moyoni kuhusu tukio la mume wake kutekwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni