Kama utakumbuka hivi karibuni rapper 50 Cent alikuwa katika steji ya Baltimore ambapo alinaswa na kamera za mapaparazi akimtwanga ngumi shabiki wakike ambaye alikuwa akimvuta 50 Cent, kupitia ripoti kutoka mtandao wa Tmz, umesema kwamba mwanamke aliyepigwa ngumi na 50 anajulikana kama Donetta Derr na ameamua kumshitaki 50 cent pamoja na crew nzima ya show hiyo ya Baltimore.
Taarifa zinasema kwamba baada ya tamasha hilo kuisha, siku iliyofuata
derr aliamua kwenda hospitali ambapo huko aliamua kuja na uamuzi wa
kumfungulia mashitaka 50 cent, sound steji ya Baltimore na wote ambao waliperforme kwenye show hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni