EPL hakuna mpira wa mezani - Niki wa Pili

Msanii kutoka kampuni ya Weusi Niki wa Pili amefunguka ya moyoni kutokana na ushindi walioupata Manchester United usiku wa jana na kusema ni bora aendelee kushabikia mechi za EPL zinazoendelea kuliko kujihusisha na ushabiki mpira wa Tanzania

Ambao unaonekana kuwa na figisu figusu nyingi

Hayo yameibuka baada ya kelele nyingi nchini kufuatia timu ya Simba kupewa alama 3 kutoka kwa Kagera Sugar kutokana na kile kinachoaminiwa na mamlaka husika kuwa walimchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

“Tunapenda EPL kwa sababu mpira unachezwa uwanjani. Bongo mpira mnataka kuucheza nje ya uwanja, bla bla tupuu.. Ligi ya kulevya”. Ameandika msanii huyo kupitia twitter yake

Mbali na Niki wa Pili kuna watu wengi wamechukizwa na kitendo cha timu ya msimbazi kupewa ushindi mezani, huku wengine wakisema ndiyo sababu ya kudharaulika kwa michezo ya nyumbani.
Share:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Social