Akiongea na eNewz ya EATV Kala Jeremiah
amesema awali watu walipomwambia alishtuka na hakuamini lakini baada ya
kutazama marudio ya kipindi aligundua Dayna aliongea kwa utani na wala
hakutegemea kama ingekuwa ni story kubwa na kusisistiza kuwa wao ni
washkaji hakuna hata ugomvi unaoendelea kati yao.
"Sitaki kuamini kama Dayna
hanifahamu. Sisi ni washkaji wa muda na hata alivyodai hanifahamu huwezi
amini sijawahi kumpigia simu nimuulize maana tunakutana na tunapiga
story kama kawa. Hicho siyo kitu kikubwa sana kwangu cha ku-mind kwa
nini anikane, kwa sababu kwanza kila mtu anajua ushkaji wetu uliopo kati
yangu mimi na Dayna na ukizingatia mimi ni mmoja kati ya marafiki zake
wanaoimba hip hop" Amesema Kala Jeremiah.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni