Kamati ya saa 72 iliyokaa kikao leo April 13 na kuamua kuhusu malalamiko ya
Simba kwa
Kagera Sugar kuhusu kumtumia mchezaji
Mohamed Fakhi katika mchezo dhidi yao April 2 2017 akiwa na kadi tatu za njano kinyume na taratibu na kanuni za Ligi.
 |
Mohamed Fakhi picha hii ni wakati akiwa mchezaji wa Simba |
Simba walipeleka malalamiko hayo katika bodi ya Ligi na
kuomba ipitie ripoti za waamuzi ili kujulikana ukweli, leo April 13
kamati ya saa 72 chini ya mwenyekiti wake
Hamadi Yahaya ilikaa na kujiridhisha kuwa
Kagera walikiuka taratibu hizo kwa mujibu wa Kanuni
Simba wamepewa point zote tatu za mchezo dhidi yao.
Kamati imejiridhisha kuwa mchezaji
Mohamed Fakhi alioneshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya
Majimaji,
Mbeya City na
African Lyon, hivyo hakustahili kucheza katika mchezo dhidi ya
Simba uliyochezwa April 2 2017 uwanja wa
Kaitaba na
Simba ikapoteza kwa magoli 2-1.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni