Kutoka nyanda za juu pande za green city mbeya mwanamuziki
wa muziki kizazi kipya petronia yahya mfaume amezungumzia ujio wa ngoma yake
mpya japo hajataja jina la hiyo ngoma wala siku ambayo atakupa nafasi wewe shabiki wa
muziki wa mwanadada huyo kuisikiliza kwa mara ya kwanza ngoma hiyo.
Akizungumza na rock fm kwenye kipindi cha ngoma time petronia alisema
“hivi karibuni ntaachia ngoma yangu
ambayo kwa sasa siwezi kusema inaitwaje lakini ni new project inayofuata baada ya kazi zangu ambazo
zimepita na kama unakumbuka vizuri ngoma yangu ya mwisho kuachia ilikuwa ni
cover ambayo ilikuwa inaitwa nilipize ya ibra nation”
Ameongeza kwa kusema “
ngoma yangu mpya nimeifanya katika studio za E-record na producer j willz ni
habari njema kwa mashabiki zangu kwa kipindi kirefu sana nimekuwa kimya so
nimerudi na ngoma yangu mpya mengi zaidi mtayajua baada ngoma yangu kutoka
sababu ipo jikoni inapikwa very soon itatoka”
Hiyo ndio habari mpya kutoka kwa petronia kwa mashabiki wake
so get ready.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni