Msanii wa kike wa hip hop bongo Chemical, kwa mara ya kwanza
amezungumzia maisha yake ya kimapenzi, kitu ambacho ni nadra sana kwa
msanii huyo kufanya hivyo.
Chemical amesema yeye kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua
kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala
ya mapenzi.
“Unajua kuna mambo mengine tunayafanya kwenye muziki kuweza kuweka
image nyingine, ila mi niko tofauti na niko real, ukisikiliza nyimbo
zangu nyingi Chemical anajua kupenda, anataka kubembelezwa, mi msichana
jamani, na mapenzi yapo, ila mimi nahisi nina vitu vini vya kufocus
kiasi kwamba kwenye mapenzi sitii nguvu nyingi, sipendi moyo wangu
uumie”, amesema Chemicla.
Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa
akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi
cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba
alisaini naye mkataba.
Home »
» “Mimi ni msichana nataka kubembelezwa” - Chemical
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni