Akizungumza na eNewz baada ya kuwepo na maswali ya wapenzi wa muziki mtaani kuanza kuhoji namna ya ufanyaji kazi wake kuwa tofauti na jinsi soko la muziki wa bongo unavyofanyika hasa katika suala zima la kutafuta kiki na kuzungumziwa.
"Mimi sioni kama nina tatizo lolote na wala sijutii kabisa kutokuwa kwenye 'trending' ninachoangalia ni kama muziki wangu unaenda na mashabiki zangu wanauelewa hilo ndio la msingi kwangu na muziki wangu ukiangalia uko poa na watu wanauelewa so hayo mambo ya trending kwangu sio issue" Izzo
Izzo Bussiness kwa sasa anafanya vizuiri na ngoma mpya inayoitwa Saa Sita baada ya mwezi Disemba kuachia wimbo wa Baraka kama zawadi kwa mashabiki zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni