Mkali wa HipHop Bongo Fid Q ameonekana kukamatika kimahaba kwa mrembo
ambaye ameshamtambulisha nyumbani kwao Mwanza na kwa
sasa yupo kwenye mahusiano nae rasmi.
Fid Q amesema ameamua kupost picha kwenye mitandao yake ya kijamii
ili kupunguza wasichana wengine kumtumia meseji za kumsumbua lakini pia
kuwaonyesha mashabiki zake kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi
kwani umri wake unaruhusu.
''Nimeamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kuzuia usumbufu wa kina
dada wanaonisumbua katika mitandao ya kijamii na hata ninapokuwa kwenye
viwanja vya starehe na mda wowote kuanzia sasa ninaweza kutangaza
ndoa'', amefunguka.
Kwa upande wake mrembo huyo wa Fid amesema hawashangai sana wanawake
wanaomtongoza Fid kwenye 'Social network' kwa kuwa mpenzi wake
anamuonekano mzuri na ni mwanaume ambaye ameshapitia mambo mengi duniani
hivyo anaamini kwamba atakuwa mwanaume bora kwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni