'Hitmaker' wa Ngarenaro, Dogo Janja amemchana msanii Edu Boy kwa aina
yake ya uimbaji ya kuwa-diss wasanii wenzake katika mashairi yake na
kudai kuwa anachokifanya ni utoto mtupu na kwamba hawezi kufaidika na
lolote.
Dogo Janja amesema kwamba msanii anapaswa kuimba kitu ambacho hata
kizazi kijacho kikipata fursa ya kuskiliza nyimbo zao kitajifunza kitu
kupitia mashairi ya msanii husika.
Dogo Janja ameendelea kusema kwamba "mpaka sasa tunasikiliza nyimbo
walizoimba wasanii wa zamani kama kina Mbaraka Mwinshehe kwa kuwa
waliimba nyimbo zenye maadili na zenye ujumbe kwa jamii lakini pale
unapoamka na kuanza kuandika mashairi ya kumchana msanii mwenzio huwezi
kuwa na historia nzuri kwenye sanaa".
Msanii huyo amedai kwamba Edu Boy ni kama mdogo wake kwenye sanaa kwa
kuwa amemkuta kwenye sanaa na kusema kuandika wimbo unaowachana wasanii
wezake inakuwa kama umeamka na mawazo yako alafu unaamua kuyamalizia
kwa wasanii wezako kwani anachoamini ni kwamba hata ukiwachana wasanii
wezako huwezi kufaidika kwa lolote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni