Wakazi
amebainisha hayo ikiwa ni siku moja kupita tokea apate kura nyingi
zilizopigwa na wananchi kwa kumchagua msanii wanaomkubali baina ya hao
wawili.
"Godzilla mimi haniwezi
kwenye kuandika hata free style ila mimi ninampa tu heshima yake ya
ku-free style kama ninavyompa Nikki Mbishi. Ana mapungufu mengi tu
kuyaelezea lakini kama ametaka tumeamua kuyaelezea ila tu asijisumbue na
'body of work' nina kazi nyingi 'mix stape' sita, albamu tunatafuta tu
mazingira ya kuzitoa 'maybe' mazingira yenyewe ndiyo haya sasa " alisema Wakazi
Pamoja na hayo, Wakazi amesema si kweli
kwamba anamuonea Godzilla kwa kuwa ametambua ana msongo wa mawazo kwani
hata yeye mwenyewe pia anatatizo hilo pia linalomsibu kwa upande wake
hivyo amemtaka aache visingizio visivyokuwa na nguvu.
"Mimi sijui Godzilla
anapitia vitu gani sasa hivi lakini mimi mwenyewe nina msongo wa mawazo
nina binamu yangu amelazwa Muhimbili anahitaji figo na mpaka sasa sijui
nafanyaje 'so' hakuna asiyekuwa na mawazo, kwenye muziki huwezi kusema
kwamba hiki ndiyo kipimo cha mafanikio au ndiyo kipimo cha mtu huyu
anaweza au hawezi kwa sababu kama hivyo yeye ndiyo anasemekana ndiyo
'the best in free style' halafu sasa inakuaje naaambiwa namuonea au
ndiyo inawezekana alishinda wakati mimi sikuwepo?" alisisitiza Wakazi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni