Roma Mkatoliki anadai kuwa kidole hicho kilivunjika lakini hata baada ya kufanyiwa matibabu bado kidole hakijaweza kukaa sawa kwani kimekuwa hakina mawasiliano lakini hakiwezi kumzuia yeye kuendelea na michakato mingine akiamini kuwa ipo siku atapata wataalam ambao wataweza kukinyoosha kidole hicho.
"Unajua niliumia sehemu
nyingi ila sehemu ambayo bado haijakaa sawa ni kwenye kidole kwani
nilivunjika kwenye kidole cha mwisho tunachokiimba kilivunjika ndiyo
maana utaona nilikuwa na muongo muda mrefu zaidi ya wiki sita,
tumefungua hongo lakini kama hakijaunga bado hivyo ni kama hakina
mawasiliano hakikunji wala hakifanyi chochote, lakini hiki hakinizuia
mimi kufanya mambo mengine, Inshalaah kila kinachotokea Mungu huwa na
sababu zake labda Mungu hapendi ninyooshe kidole cha mwisho juu tena
jukwaani japo siamini katika hilo panapo majaliwa tutapata wataalam
wakinyooshe kitakaa sawa" alisema Roma Mkatoliki
Mbali na hapo Roma Mkatoliki anasema mtandao wake wa Instagram ulikuwa 'hacked' siku mbili baada ya wao kuachiwa huru na mateka hivyo saizi anahangaika kuhakikisha wanairudisha account yake hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni