Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake
ameonekana kushindwa kutumia lugha ya staha huku akionesha kutokwa na
povu jingi kutokana na mapokeo ya mashabiki wa filamu ambao walio wengi
wamekuwa wakiwachana wasanii hao na kuwataka kufanya kazi zenye ubora.
Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema
kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao waliandamana ni matahira kwani
kitendo cha wao kutaka filamu za nje zizuiliwe hakina tija na mantiki
yoyote.
Kutokana na jambo hilo, ndipo hapo msanii huyo alipoamua kushusha ujumbe kwa msanii Nay wa Mitego
"Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo
umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana
wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa....acha kupotosha jamii
yetu Kwa sababu zako binafsi... sisi wasanii hatujakataza movie za nje.
Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa
biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano" alisema Mlela
Mbali na hapo msanii huyo pia ameomba mpambano na Nay wazichape
"Nay wa Mitego acha kutafuta
sifa... nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo
msanii...halafu huwezi kufananisha filamu na muziki..... Wewe si mtoto
wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing
kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu..... This is
serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za
kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale" Yusuph Mlela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni