Steve
Nyerere amesema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kusema ni kweli
kulikuwa na matatizo hapo nyuma lakini matatizo hayo siyo sababu wao
kuharibu undugu wao na urafiki wao, hivyo ule ulikuwa ni upepo na
umepita kwa sasa wanaendelea kuishi kama zamani.
"Wema hawezi kuwa adui yangu
Wema ni rafiki yangu, Wema ni ndugu yangu hivyo yeye kuhama chama na
kuhamia CHADEMA si kubadilisha urafiki, na kuhusu matatizo na Mama Wema
yule ni mama yangu kwa hiyo yaliyopita si ndwele tugange yajayo, mimi na
wewe ni ndugu yangu kabisa na tumeshakutana mara kwa mara baada ya yale
kutokea na maisha yanaendelea. Wema na mama yake ni ndugu zangu wale
siwezi kuwatupa sijakosana na mtu Wema ni dada yangu, rafiki yangu
kipenzi na mama ni mama yangu mzazi yale yalipita ule ni upepo tu" alisisitiza Steve Nyerere
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni