Hivi karibuni Nenga amefunguka hayo wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari na kudai kuwa ameingiza hela nyingi kupitia shows, ringtone pamoja YouTube.
“Mungu ni mwema sana,
‘Mazoea’ imefanya mambo makubwa sana katika maisha yangu, na ni wimbo
ambao umeniingizia hela nyingi sana kuliko nyimbo zangu zote,” alisema Billnass.
Billnass ameogeza kuwa “Mauzo
ya mitandaoni yamekuwa makubwa sana, shows nyingi ambazo nimekuwa
nikifanya nalipwa vizuri, YouTube. Yaani huu wimbo umekuwa kama baraka
katika maisha yangu. Siwezi kusema nimeingiza kiasi gani lakini ni hela
nyingi sana"- Billnass aliendelea kufunguka.
Wimbo wa huo wa 'Mazoea' Billnassa ameshirikiana na rapa Mwana FA, umeangaliwa mara 877,121 kupitia mtandao wa YouTube kwa kipindi cha miezi 4.
Hata hivyo Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio mpya ambao amedai utakuwa na surprises nyingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni