Rapper na producer LAST BORN
kutoka nyanda za juu kusini GREEN CITY MBEYA chini ya usimamizi wa
record rebel ya T-MOTION baada ya kukaa kimya kwa muda ametuletea mixtape.
Rapper huyo amejitosa
katika soko la mixtape na kuisogeza MY STORY mixtape karibu kabisa na sikio
lako japo ramani ya muziki kwa sasa inaonekana kupoteza njia kutokana na kuwepo
kwa upepo unaovuma kwa kasi katika anga la siasa lakini hiyo sio changamoto
kwenye mixtape ya rapper last born .
Mixtape hiyo ambayo imetoka hivi karibuni na kubatizwa jina
la MY STORY imekamilishwa na ngoma 14 Huku ikiwa na wasanii wakubwa zaidi ya
kumi walioshirikishwa ndani ya mixtape
hiyo akiwemo rapper country boy ,
selementary , zax 4real , nemo , makanta
jr , jadah makanta ,adamore, young boys gorko flow na dasi.
Mixtape hiyo ipo chini ya maproducers saba waliofanikiwa
kutengeneza hits kibao katika ramani ya
muziki wa bongo freva akiwemo GACH B, J
WILLZ, S2 KIZZY, DAMOST, ROPA BEATS, OLD PAPER, NACH B akiwepo na yeye mwenyewe
LAST BORN kutoka T-MOTION.
Pia mixtape hiyo inapatikana kwa TSH 5000 kuwa mjanja kwa
kukamata nakala yako ili kuweza kuinua muziki wa hiphop kutoka nyanda za juu
kusini wacheki hapa T-MOTION no; 0625685817,0718790349, na 071229500.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni