MBEYA CITY YAMPA JEURI MINGANGE

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Sokoine, Kocha Mkuu wa  Ndanda, Meja Mstaafu wa Jeshi, Abdul Mingange, amesema ushindi huo umewapa jeuri ya kuendeleza kugawa dozi kwa michezo iliyosalia.


Meja Mingange alisema uwepo wake katika kikosi hicho anayaona mafanikio makubwa  baada ya timu hiyo kupanda nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo.

Meja Mingange alisema mafanikio hayo yanatokana na usikivu wa wachezaji anapokuwa nao kwenye mazoezi.

Meja Mingange alisema kutokana na ushindi huo, umeifanya timu hiyo kushika nafasi 10 kutokana na pointi 30.

“Tunafurahia ushindi wa (jana) juzi ambao umetupa nguvu na morali ya kupambana zaidi, hivyo tutajitahidi kila njia angalau tushinde kwenye michezo yetu iliyobaki ambayo kidogo itatupa moyo zaidi wa kujiweka pazuri kwenye msimamo,” alisema Mingange.
Share:

Related Posts:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Social