Soko la album kwa sasa kidogo limeanza kuonekana linarudi
kwenye thamani yake ni kutokana na wasanii wengi sana kuonekana kutilia mkazo kutoa album
kuliko kipindi cha nyuma hii yote ni kutaka kuweka heshima na kutaka kujiongezea kipato kwenye biashara
ya muziki.
Mtafya anapenda kuwataarifu mashabiki wa muziki wake kuwa siku ya ijumaa ya tarehe 12/05/2017 ndio itakuwa siku rasmi ya uzinduzi wa album aliyoipa jina la kutukuyu kusouth albam inayokamilishwa na ngoma kumi uzinduzi huo utafanyika pale GR CITY HOTEL kwa kiingilio cha TSH 5000 pia amesema kabla ya
kuachia albam hiyo ataachia ngoma mpya ambayo itakuwepo kwenye album hiyo.
Pia amewatoa hofu mashabiki wa muziki wake watakaofika kwenye uzinduzi huo kuwa hali ya usalama itakuwa poa. uzinduzi huo utahudhuriwa na viongozi wakubwa wa mkoa wa mbeya akiwemo RPC wa mkoa wa mheshimiwa kidavashari na muheshimiwa mkuu wa mkoa wa mbeya ndugu amosi makala
Aidha abum hiyo itauzwa kwa TSH 5000 tu pia kwenye album hiyo kuna mengi mazuri amekuandalia zikiwemo ngoma kali ambazo ameshaziachia na ambazo hujawahi kuzisikia kabisa ukiikosa utakuwa hujautendea haki sikio lako la kiburudani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni