Msanii wa kike wa muziki bongo Lulu Diva amefunguka tuhuma za kuachwa na
mpenzi wake wa muda mrefu, na kunyang'anywa vitu ambavyo alimnunulia.
Lulu Diva amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, ingawa ni kweli
kulitokea kutoelewana na mpenzi wake kutokana na msanii anayejulikana
kwa jina la Richad, lakiini ana amini yatakwisha na wataelewana.
“Ni vitu ambavyo vimetokea lakini siwezi kuviongelea sana, ila
nikwamba jamaa siko kwenye mahusiano naye, kwa hiyo mpenzi wangu
vimekuwa kwake ni tofauti kuolewa lakini I hope soon tutakaa sawa,
kuhusu kunyang'anywa vitu sio kweli sijanyang'anywa na hawezi kufanya
hivyo, ilikuwa tu ni ugomvi”, amesema Lulu Diva
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva yupo kwenye mahusiano
na msanii moja hapa bongo kiasi cha kuvuja kwa picha wakiwa kwenye pozi
za mahaba, kitendo ambacho kimeonekana kumchukiza mpenzi wake wa siku
nyingi ambaye hajulikani kabisa mitandaoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni