Msanii wa muziki wa hip hop, Roma
Mkatoliki, Moni pamoja na wenzao 2 leo wanatarajiwa kueleza sakata zima
la tukio la kutekwa kwao wakiwa studio za Tongwe Records Masaki, jijini
Dar es Salaam.
Wasanii wanaodaiwa kutekwa ambao
wataungana na Roma katika mkutano na waandishi wa habari leo ni Moni
Centrozone, prodyuza wa studio hiyo, Bin Laden na mfanyakazi wa mama
mzazi wa mmiliki wa studio hiyo, Junior Makame (J Murder), anayefahamika
kwa jina la Imma.
Juzi usiku baada ya kuruhusiwa kutoka
Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam na kufanyiwa uchunguzi katika
Hospitali ya Mwananyamala, Roma aliwaambia waandishi wa habari kwamba
atazungumza leo.
“Mi ni mzima kabisa, nipo vyema kiafya
na kiakili na wenzangu watatu nikimaanisha Mon, Bin Laden prodyuza wetu
pamoja na Imma mfanyakazi wetu pale Tongwe; wote tu wazima tunaendelea
vizuri, kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa za tukio zima
ambavyo limetokea.
“Lakini taratibu hizo zinatufunga
tusiweze kuongea chochote kwa sasa hivi, lakini ratiba naweza kuwapa
kushinda kesho Jumapili, Jumatatu nadhani ndiyo kutakuwa na ‘Press
Conference’ kukutana na kuongelea kuhusu hiyo stori, mturuhusu tu
tukapumzike nawashukuru, niseme tu asante,” alisema Roma.
Roma na wenzake walitekwa Jumatano wiki hii wakiwa katika studio za Tongwe Recods iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni