Hayo yameibuka baada ya Msami kumtaka AT
aboreshe kazi zake badala ya kulalamika kuwa kuna watu wanaobebwa huku
akijitapa kuwa dancers wana maisha mazuri na mafanikio makubwa kumzidi
yeye.
“Hawa watoto huku kwangu
siyo pakuchezea, mchezeeni Alikiba mnyonge anakaa kimya hata mkimtukana
hajibu kitu ila huku kwangu waachane napo siyo kwa kawaida na kama
hawataki basi wajaribu zali kama wenzao halafu watapata majibu yao”. Alisema AT
Aidha AT alifika mbali zaidi kwa kusema
yeye ni msanii bora kuliko anavyomchukulia kwa kuwa anaweza kucheza na
‘vocal sound’ kwa kuiga sauti wasanii wakubwa huku akitolea mfano kwa
Bi. Kidude, Oliver Mtukuzi pamoja na Chriss Brown
“Wewe hunijui, umeenda tu
kuruka ruka sehemu umechukuliwa baadae umejiona umeimba chooni ukadhani
unajua kuimba. Mimi mwenzio nimeenda chuoni”. Alisisitiza AT
Mbali na hilo AT aliwataka watu ambao
wanatafuta majina kupitia yeye wakome kabisa tabia hiyo kwani yeye ni
mtu mbaya akisema siku aachie mabomu yake hawataweza kuvumilia kwani
watatafutana, hivyo kama wanataka kiki waende kwa Harmorapa lakini si
kwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni