PRODYUZA maarufu, Suge Knight, ametoboa siri kuwa waliohusika katika
mauaji ya mwanamuziki Tupac Shakur ni watu wawili akiwamo mke wake wa
zamani, Sharitha.
Tupac alifariki mwaka 1996 baada ya kupigwa risasi jijini Los Angeles.
Suge ambaye alikuwa mtendaji mkuu wa ‘lebo’ ya Death Row Records
iliyokuwa ikimmiliki Tupac, alisema mkewe Sharitha alishirikiana na
aliyekuwa mlinzi mkuu wa studio hiyo, Reggie White Jr.
Aliongeza kuwa yeye ndiye aliyekuwa mlengwa wa tukio hilo la kupigwa risasi lakini hakuwa eneo hilo.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Daily Mail ulimuhoji mwanasheria wa Suge, Thaddeus Culpepper, ambapo alisema: “Knight
amekuwa akifahamu kwa miaka mingi kuwa Reggie Wright Jr. na mke wake wa
zamani, Sharitha walikuwa nyuma ya mauaji ya Tupac na walijaribu kumuua
Knight.”
Kwa mujibu wa Suge, Wright pia alihusika katika mpango wa kumuua Notorious B.I.G.
Hata hivyo, bado Suge hajaweka wazi majina ya waliompiga risasi Tupac.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni