Msanii wa bongo anayehit na ngoma ya 'Down', Quick Rocka amefunguka ilivokuwa mpaka akaamua kumshirikisha Mimi Mars kwenye wimbo wake mpya ambao kwa sasa unafanya poa masikioni mwa mashabiki zake
Quick amesema kuwa alishawishika kumshirikisha msanii mchanga
anayekuja kwa kasi 'Mimi Mars' baada ya kupewa sifa na rafiki yake wa
karibu.
"Unajua wakati naandaa huu
wimbo wa Down nilikuwa nipo na Jux yeye ndo akanishauri kwa nini humu
usimuweke Mars? hapo mimi sijawahi kumsikia kabisa lakini kwa vile mimi
namuamini Jux ni mzuri kwenye uimbaji na ni rafiki yangu nikaamua kumpa
Mars nafasi hiyo na yeye kama wimbo unavyousikia hakuchezea bahati.
Wimbo huu niliufanya toka mwaka jana kabla hata hajatoa wimbo wa Shuga." alisema Quick Rocka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni