Baada ya kuweka rekodi ya kuuza kopi laki 6 katika album yake ya “Damn” kwa wiki ya kwanza, kushinda studio kwa maproducer inaweza kuwa ni sababu ya kuweka rekodi hiyo.
Damn ya Kendrick Lamar iliachiliwa
rasmi tarehe 14 ya mwezi wa 4 ambapo mpaka kufikia hii leo album hiyo
imefanikisha kuweka rekodi kubwa kwa mwaka 2017 kwa kuuza nakala laki 6,
sasa moja ya sababu kubwa ambayo inatajwa kumfanya Kendrick Lamar kufikia
hapo kwenye album hiyo ni kwamba maproducer wote waliotengeneza ngoma
hiyo kila mmoja alishinda kutwa nzima studio mpaka ngoma inapoisha na
kukubalika na washikaji wote.
Kupitia Interview aliyoifanya producer SounWave na GQ,
alisema kwamba, Kila producer alitakiwa kuwa na mabegi yake kwa ajili
ya kushinda studio, yaani hakuna kurudi home hiyo mpaka ngoma
itakapokamilika na wote wakaikubali, kama mtu alikuwa na demu wake
ambaye alihitaji kuja kumwona basi alipaswa kuja studio, mashabiki
wamefunguka sababu hiyo ndio kama iliyomfanya Kendrick kupata rekodi hiyo, ndani ya Album hiyo tunakutana na maproducer kibao kama Mike WiLL Made-It, DJ Dahi, Alchemist, 9th Wonder, na Steve Lacy ambao wote hao wameshinda studioni mpaka mzigo kukamilika na kupata mafanikio haya.
Home »
» Hii inaweza kuwa ni sababu ya Kendrick Lamar kufanya vizuri kwenye album ya ‘Damn’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni